Kulingana na Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -Abna- Marajii Taqlid Wakuu katika Ulimwengu wa Kishia, Ayatollah: Sistani, Makarem Shirazi, Nouri Hamedani, Javadi Amoli, Sobhani na Shabiri Zanjani, wameshutumu vikali katika taarifa na kauli tofauti matamshi ya udhalilishaji ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ayatollah Makarem Shirazi:
Uwepo wa Kiongozi kama Mlinzi wa kuhifadhi uwepo wa Ushia, na hata wa Umma wa Kiislamu, ni hatua nyeti katika imani yetu, na hakuna Muislamu Mwema na aliye huru anayeweza kuvumilia tishio hilo (la Trump).
Ayatollah Sistani:
Unashutumiwa vikali uvamizi wa kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na tishio lolote lenye nia ovu dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Kidini na Kisiasa wa nchi hii.
Ayatollah Nouri Hamedani:
Kila aina ya uvukaji mipaka dhidi ya Kiongozi Mkuu na Kiongozi wa Umma wa Kiislamu unachukuliwa kama uvunjaji na uvukaji wa msingi wa Uislamu na kwa nafsi za Waislamu wote, na hilo litakabiliwa na majibu makali na yenye nguvu ya watu wote wa Iran na pia watu wote Walio huru wa ulimwengu mzima.
Ayatollah Javadi Amoli:
Iran ya Kiislamu, watu wote, wanasayansi na viongozi wa kijeshi na kisiasa wa ngazi za juu, na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ambaye ndiye kitovu cha uhuru na nguzo ya uthabiti (istiqama), wote wawe salama chini ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu.
Ayatollah Sobhani:
Katika hali hii nyeti ambayo iko wazi kwa kila mtu, ni wajibu wa wasomi wa Kiislamu na viongozi wa kidini katika maeneo yote ya ulimwengu kukemea uvamizi wa ukafiri kwa ulimwengu wa Kiislamu, na wote watoe wito kwa sauti moja kukomeshwa kwa uvamizi huo.
Ayatollah Shabiri Zanjani:
Utawala huu (wa Kizayuni) umevunja kwa uwazi kabisa haki za msingi za binadamu, umekuwa ukifanya mauaji ya wanawake, watoto, watu wasio na hatia, askari na wasiokuwa askari, na sasa unatoa tishio dhidi ya Kiongozi Mkuu wa ngazi ya juu. Katika hali hii nyeti, uhifadhi wa umoja wa kitaifa, utambuzi, nia nzuri, mshikamano wa Waumini, na msaada kwa kila mmoja ni silaha kubwa dhidi ya vitisho hivi, na ni wajibu wa wote walio na kalamu na taasisi za kimataifa kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia ukiukaji huu muovu na uharibifu usio weza kufidiwa.
Your Comment